Jumanne , 2nd Dec , 2014

Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI mkoani Kilimanjaro kimeongezeka kutoka asilimia 1.9 kwa mwaka 2010/2011 hadi kufikia asilimia 3.8 mwaka 2013/2014 ikiashiria bado jamii haijabadili tabia.

Akiongea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambapo kimkoa yamefanyika kijiji cha Rundugai, kata ya Masama Rundugai wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Mganga mkuu wa mkoa wa Dkt Mtumwa Mwako amesema licha ya jitiada mbalimbali zinazo fanywa na serikali bado tatizo la UKIMWI ni sugu.

Ukimya huu ukavunjwa na wananchi wa jamii ya wafugaji wanao ishi mipakani kati ya wilaya ya Siha mkoani hamo na Longido mkoani Arusha, wakati wakimsimika kiongozi wa kimila Legwanani Sembeta Msanga wa ukanda wa odimeti, ambapo wamesema miaka mingi imepita na hawajawahi kupata elimu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI.

Naye Mratibu wa UKIMWI wilaya Bw. Robati Mwanga amesema kama halmashauri imeandaa mikakati madhubuti ya kuhamasisha wananchi katika kupambana na ugonjwa wa UKIMWI.

Kauli Mbiu ya mwaka huu, Tanzania bila maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana.