Jumapili , 2nd Aug , 2015

Maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana wa kike wenye umri wa kati ya miaka 15 na 39 mkoani mbeya yameongezeka kwa zaidi ya mara tatu ikilinganishwa na vijana wa kiume wenye umri kama huo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Utafiti huo umefanywa na tume ya taifa ya kudhibiti ukimwi, TACAIDS , umebaini kuwa kasi ya maambukizi ya ukimwi kwa vijana wa kike mkoani mbeya ni kubwa ikilinganishwa na vijana wa kiume.

Akizungumza na mkoani mbeya mratibu wa ukimwi mkoani humo , stella kategile ameeleza sababu ya kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa mtoto wa kike mkoani mbeya kuwa juu ikilinganishwa na mtoto wa kiume

Ameongeza kuwa wazazi wamekuwa hawatoi kipaumbele kwa watoto wa kike haswa pale wanapofeli masomo yao na hivyo kuwaacha pasipo kuwajengea au kuwapa nyenzo za kuwasaidia kujiendeleza katika maisha yao hivyo wengi kuishia katika makundi rika ambayo hayana elimu ya tahadhari kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Kwa mujibu wa takwimu za kitaifa, mkoa wa mbeya unashika nafasi ya tatu kwa kuwa na maambukizi makubwa ya ukimwi nchini, ukitanguliwa na mkoa wa dar es salaam na iringa.