
Ndege za Shirika la Ndege la Ujerumani Lufthansa.
Shirika hilo la ndege linakabiliwa na siku mbili nyingine za mgomo wa marubani wiki hii, baada ya chama cha wafanyakazi marubani kusema kuwa awamu ya hivi karibuni ya mazungumzo juu ya nyongeza ya mshahara imeshindwa.
Marubani waligoma kwa muda wa siku nne wiki iliyopita, wakisababisha kiasi ya wasafiri 300,000 kukwama na kusababisha hasara ya mamilioni ya euro.