![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2022/11/04/Untitled-1_3.jpg?itok=AcRT8gbS×tamp=1667584895)
Mashahidi hao wawili ambao ni daktari aliyempima mtoto wa mchungaji huyo Pamoja na mpelelezi wa kesi hiyo wameshindwa kufika mahakamani baada ya kuwa majukumu mengine ya kikazi hali iliyopelkea kushindwa kufika mahakamani hapo na kupelekea hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Magu Erick Kimaro akalazimika kuiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 14 ya mwezi huu
Ikumbukwe kuwa Mchungaji Nurdin Abdalah anadaiwa kumbaka kwa nyakati tofauti binti yake mwenye umri wa miaka 6 mara baada ya kuachana na mama yake mzazi mnamo mwezi wa saba mwaka huu ndipo mwezi wa nane majirani wakabaini kwamba binti huyo amaekuwa akiingiliwa kimwili na kumdadisi na kusema baba yake huyo ndiyo amekuwa akimuingilia usiku wakati wakiwa wamelala na kumkataza kusema kwa watu