Jumatano , 24th Nov , 2021

Mkoa wa Kagera utapoteza zaidi ya shilingi Bilioni 53.4 kwa mwaka, zinazopatikana kutokana na mauzo ya dhahabu, endapo wilaya za Ngara na Biharamulo zitamegwa kwa ajili ya kuunda mkoa mpya wa Chato.

Sehemu ya eneo la mkoa wa Kagera

Amesema Katibu Tawala Msaidizi Menejimenti na Serikali za Mitaa mkoa wa Kagera, David Lyamboka, wakati akizungumza katika kikao cha kujadili na kushauri serikali juu ya faida na hasara zitakazotokana na wilaya hizo kumegwa.

Aidha amesema kuwa pia mkoa wa Kagera utapoteza shilingi bilioni 3.7 ambazo zinatokana na mapato ya ndani ya mamlaka ya serikali za mitaa, hali ambayo itasababisha mkoa huo kuendelea kuwa wa mwisho katika mikoa masikini.