Alhamisi , 3rd Aug , 2017

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzania Thobias Andengenye amewaapisha maofisa wawili wa jeshi hilo walioteuliwa na Rais John Pombe Magufuli hivi karibuni kuziba nafasi za juu zilizoachwa wazi kwa muda wa zaidi ya miaka 2

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha maofisa hao, ambao ni Kamishna wa Divisheni ya Oparesheni Kamishna Billy Mwakatege, na Kamishna wa Divisheni ya Usalama wa moto Kamishna Jesual Ikonko, amesema wanalenga kuona huduma za uokoaji na zimamoto zikiboreshwa huku elimu ikitolewa kikamilifu kwa wananchi ya namna wanavyoweza kujikinga na majanga ya moto.

"Nijukumu lenu kuhakikisha kuwa ufanisi unaboreshwa, mfanye kazi kwa viwango vya kimataifa ikiwemo kuboresha mifumo ya jeshi la zima moto pia mlinde mali za jeshi hili, na zaidi muhakikishe kuwa wananchi wanatambua wajibu wao katika kujikinga na mjanga ya moto" amesema Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzania Thobias Andengenye

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya Moto, Jesuald Ikonko.

 Aidha, Kamishna Generali Thobias Andengenye amesema, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linalenga kuunda vikundi vya Zimamoto mashuleni hususani shule za sekondari kwa lengo la kutoa elimu kwa wanafunzi ili kujenga taifa lenye uelewa wa kujikinga na majanga ya moto na kujiokoa.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa, Kamishna wa Divisheni ya Oparesheni Mwakatege ameelezea vipaumbele vyao na namna walivyo jipanga kufanya maboresho ya kiutendaji katika nafasi zao ndani ya Jeshi la Zimamoto na uokoaji.

"Katika nafasi ya uongozi nitaanza na oparesheni ya ukaguzi wa miundombinu ya moto hasa kwa majengo makubwa yaliyopo katikati ya jiji, ili kuhakikisha kuna kuwa na usalama wa mali na watu wao na kuepuka vifo visivyo vya lazima" Kamishna wa Divisheni ya Oparesheni Billy Mwakatege.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Operesheni Billy Mwakatage