Jumatano , 25th Feb , 2015

Jeshi la polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutuliza vurugu kubwa zilizoibuka leo Kati ya Polisi na wananchi wa mjini wa Ilula katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kufuatia kifo chenye utata cha mwanamke mmoja.

Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 5 asubuhi Leo na kudumu hadi Majira ya saa 10 jioni huku kituo cha Polisi kikivunjwa ,bunduki kuporwa na nyingine kuchomwa moto pamoja na magari matatu na Pikipiki Moja ya polisi.

Wakizungumzia tukio hilo wakazi wa mji huo wamesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni askari watatu akiwemo mkuu wa kituo cha Ilula kwenda kufanya msako wa wananchi wanaokunywa pombe muda wa kazi.

wamesema kuwa mwanamke aliyepoteza maisha kutokana na tukio hilo aliyetambulika kwa jina la Mwanne Mtandi alikuwa akikimbia kukwepa kukamatwa na Polisi hao Kabla ya kukutwa nyuma ya jengo la klabu hicho cha pombe za kienyeji kilichopo mtaa wa Ilala Mjini Ilula akiwa amekufa.

akizungumzia tukio hilo Diwani wa kata ya Nyalumbu Ally kikunga amesema kuwa alipigiwa simu na wananchi wake kujulishwa juu na vurugu hizo na Baada ya kufika Eneo la tukio alikuta mwanamke huyo akiwa mahututi na wala hakupata msaada toka kwa wananchi wengine kwa ajiri ya kumpelekwa hospitalini .

Hata hivyo amesema Raia hao wameharibu Mali mbali mbali ndani ya kituo cha polis pamoja na nyaraka zote na kuwafungulia mahabusu wote waliokuwemo huku Lori Moja lililokamatwa kituoni hapo likilindwa kuharibiwa kuwa halina kosa.

Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya kilolo ilifika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kutoa taarifa kamili ya Mali zilizoharibiwa na chanzo halisi cha tukio hilo Baada ya kukaa kikao na viongozi wa jeshi na Polisi na wale wa mji wa Ilula.