Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya kutembelea Makumbusho ya Sayansi ya Kampuni ya Toshiba na kiwanda cha kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme cha Tsurumi kinachomilikiwa na kampuni hiyo.
Akizungumza na viongozi wa kampuni ya Toshiba, Waziri Mkuu amesema, "wawekezaji wote wanaokuja kuwekeza Tanzania wakiwemo wa kutoka Japan pamoja na kampuni ya Toshiba, watambue kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imeboresha mazingira ya uwekezaji na kuyafanya yawe rafiki, nina uhakika wawekezaji watakaoamua kuwekeza Tanzania hawatajutia uamuzi wao huo”.
Waziri Mkuu amewahakikisha viongozi hao kwamba hawatojuta kuwekeza nchini Tanzania kutokana na sera nzuri na mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara, pamoja na soko la uhakika wa bidhaa zitakazozalishwa kwa kuwa Tanzania imezungukwa na nchi nyingi.

