Jumatatu , 11th Jan , 2016

Hali ya ugonjwa wa kipindupindu katika mkoa wa Dar es salaam umeelezwa kumalizika kwa sasa baada ya kutoripotiwa mgonjwa yeyote wa kipindupindu tangu tarehe ishirini na mbili mwezi wa kumi na mbili mwaka 2015 hadi kufikia leo.

Naibu waziri wa afya , maendeleo ya jamii wazee na watoto Mh. Hamis Kigwangwala wakati akitoa ripoti kwa waandishi wa habari juu ya hali ya kipindupindu nchini Tanzania

Hayo yameelezwa na naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh. Hamis Kigwangala wakati akitoa ripoti ya hali ya kipindupindu nchini Tanzania, huku mikoa ya Mtwara, Njombe na Ruvuma ikielezwa kutoripoti uwepo wa ugonjwa huo kwa kipindi chote ambacho ugonjwa huo umekuwepo nchini.

Mh. Kigwangala amewataka wahudumu wote wa afya nchini kuendelea na jitihada za kuutokomeza ugonjwa huo nchini pamoja na kutoa rai kwa wananchi kuendelea kuyaweka mazingira katika hali safi ya kutokomeza mazingira ya ugonjwa huo hapa nchini.