Jumapili , 23rd Feb , 2025

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ametoa wito kwa viongozi wa madhehebu ya dini kuendelea kufundisha na kuimarisha elimu ya dini ili kutoa fursa kwa watoto na vijana kupata elimu hiyo na kuwaandaa kuwa watu wema. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,

Ametoa wito huo leo Jumapili Februari 23, 2025 alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha tuzo za 33 za Kimataifa za Kuhifadhi Qurani Tukufu katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. 

"Jukumu la kuhakikisha maadili bora ni la kwetu sote, madhehebu ya dini yakiwa na mchango mkubwa," amesema Waziri MKuu

Aidha, Waziri Majaliwa amehimiza madhehebu yote ya dini kuendelea kuhubiri amani, mshikamano na utulivu hasa katika kipindi cha kuelekea katika uchaguzi mkuu, "Amani na utulivu ni moja ya tunu katika nchi yetu,".

Akizungumza kuhusu tuzo hizo, Waziri Majaliwa amesema kuwa zinatoa nafasi ya kujenga maadili bora ikiwemo uaminifu, umakini, na kujitolea. “Washiriki wanajifunza umoja, upendo na mshikamano na wengine kwa ufanisi.