Serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki Pamoja na nchi nyingine Afrika zimetakiwa kuongeza juhudi katika kuwahudumia wanawake waliopata maambukizi ya virusi vya Ukimwi ili waweze Kazaa Bila kuwaambukiza watoto wanatakiwa
Katika mkutano unaowakutanisha washiriki kutoka nchi 20 za Afrika Kujadili hali pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali za nchi hizo katika kukabiliana na magonjwa ya malaria, kifua kikuu na UKIMWI.
Mkurugenzi wa bodi ya Mtandao wa Kupambana na kuenea kwa ukimwi,Kifua kikuu na Malaria eannaso katika nchi za Afrika Mashariki Marc Ndayiragiye amesema nchi za Afrika bado hazijaweka jitihada za kutosha kukabiliana na ugonjwa wa UKIMWI.
Akizungumzia hali ya wanawake wanaoishi na virusi vya UKIMWI nchini Tanzania Bi. Joan Yamungu amesema bado kiwango cha unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ni kikubwa.
Katibu mkuu wa mtandao wa watu wenye ulemavu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Fabiana Chunda ni mwanamke mwenye watoto watatu na anaishi na virusi hivyo kwa mwaka wa 11 sasa anasema kutowathamini watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kunachangia kutoonesha mchango wao katika jamii.
Watu milioni 1.8 duniani wanatumia dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI mpango unaosaidiwa na mfuko wa dunia........