Jumamosi , 23rd Sep , 2023

Mhe Rais Mstaafu Sirleaf amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuiongoza Tanzania kwa kuzingatia Demokrasi

 

Mbunge wa Viti Maalum kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Neema Lugangira ambaye pia ni mwakilishi wa Tanzania katika  Mtandao wa Dunia wa Viongozi Wanawake Wanasiasa (Women Political Leaders Org), ameshiriki mjadala wa Usawa wa Kijinsia katika Siasa, mkutano uliofanyikia New York Marekani.

Kufuatia mchango wake na jitihaza za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan alialikwa na Mhe Rais Mstaafu wa Liberia,  Ellen Sirleaf katika kikao cha faragha ambapo Mhe Rais Mstaafu Sirleaf amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuiongoza Tanzania kwa kuzingatia Demokrasia na kuimarisha usawa wa kijinsia katika siasa na huduma za kijamii.