Wanachama wa CUF
Akizungumza na EATV Digital, amesema kuwa zimeshatimia siku tatu tangu kuzuiwa kwao kufanya shughuli za kampeni katika jimbo hilo baada ya malalamiko yaliyopelekwa katika Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi juu ya ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi .
"Chama kimekata rufaa pamoja na adhabu iliyopewa na malalamiko yao wanataka ile adhabau ipunguzwe pia kwasababu siku kumi ni siku nyingi sana ikiwa ni mgombea unafanya kampeni ukaambiwa ukae tu" alisema Ali Makame Issa
Aidha Makame ameweka wazi imani waliyonayo juu ya mgombea wa chama chao katika jimbo hilo Bw. Maftah Abdallah Nachuma ambaye anatetea nafasi yake yakuendelea kuliwakilisha jimbo kuwa ni mgombea anayesubiria kuapishwa.
Hata hivyo Makame amesema kuwa wanaamini kuwa kampeni walizozuwia kufanya ni kwa upande wa Ubunge hivyo katika ngazi nyingine kampeni bado zinaendelea.