Jumanne , 22nd Oct , 2024

Katibu Mkuu Uenezi Chama cha Mapinduzi CPA Amos Makalla amesema CCM haihitaji kubebwe kwenyeMbeleko ili kuibuka na ushindi uchaguzi Serikali za Mitaa novemba 27 mwaka huu

Amos Makalla ameyasema hayo hii leo wakati akipokea ripoti ya hali ya uandikishaji ya chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amewapongeza kwa hamasa iliyofanyika katika uandikishaji na kuela mkakati wa chama hicho kuelekea hatua zinazofuata za uchaguzi ikiwemo kampeni pamoja na uchaguzi novemba 27 mwaka huu

“Jambo lingine tunaamini uchaguzi huu utakuwa huru na haki CCM itakuwa chama kiongozi cha kuheshimu matokeo yeyote aliyeshindwa ameshindwa aliyeshinda atatangazwa mshindi. Umeshinda uchaguzi kwa haki utatangazwa mshindi umeshindwa upokee matokeo hayo. Kwa hiyo CCM haihitaji mbeleko kwa kazi ilizo zifanya kwa maandalizi tuliyoyafanya tunaamini wananchi watatuelewa muda ukifika kama walivyotuelewa katika hamasa ya uandikishaji.” Amesema Amos Makalla Katibu Mwenezi Chama Cha Mapinduzi Taifa.