
Mwenyekiti wa kamati namba moya ya bunge maalumu la katiba, mhe. Ummy Ali Mwalimu
Wakati akiwasilisha mapendekezo hayo, Mhe. Mwalimu amekutana na pingamizi za hapa na pale na wengine kumshutumu kuwa hakuwa akisoma kilichoandikwa katika kumbukumbu za kikao cha kamati.
Akizungumza baada yake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Habib Mnyaa, amesema wazi kuwa Mhe. Ummy Mwalimu hakuwa akiwasilisha masuala waliyokubalina ndani ya kamati, na kusema kuwa watalinganisha alichowasilisha na kilichopo kwenye kumbukumbu za vikao na itakapobainika haikuwa sahihi kamati ya nidhamu itachukua nafasi yake.