Charles Mwijage
Kutokana na adhma hiyo, amesema taasisi hiyo inatakiwa kuhakikisha ndani ya miaka minne inakuwa na viwanda hata vitatu katika kuweza kufikia uchumi wa kati.
Mwijage ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakurugenzi NDC, amesema kuwa bodi lazima ifanye kazi kuhakikisha inashikiria viwanda vikubwa ambayo vitafanya taifa kuwa na maendeleo ya kiuchumi kutokana miradi iliyopo chini ya NDC.
Amesema kuwa mradi wa kwanza ni ule wa Liganga na Mchuchuma unatakiwa kufutika midomoni mwa watu kwa kuanza kuzalisha kutokana na muda mrefu umekuwa ukizungumzwa.
Mwijage amesema kuwa kutokana bodi hiyo kuwa na watu wa kila sekta muhimu hivyo wanahitaji kukutana mara kwa mara hata bila kulipwa posho ili mambo yaende na kuleta tija kwa taifa.
Amesema kuwa miradi mikubwa ikikamilika nchi itakuwa imepiga hatua kimaendeleo na kuweza kufikia uchumi wa kati wa viwanda vyenye kwa wananchi.
Naye Mwenyekiti wa bodi wa NDC, Dk, Samwel Nyantahe amesema kuwa watafanya kazi kwa karibu na wizara ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi yote na kuweza kuanza kufanya kazi kwa nguvu.
Amesema Rais Dk. John Magufuli amemuamini hivyo watatimiza wajibu kwa kushirikiana na bodi hiyo katika sekta ya viwanda.
Mwisho