Jumanne , 27th Sep , 2022

Wizara ya Afya nchini imependekeza kuwa bima ya afya kwa wananchi iwe ni ya lazima na si hiari, huku wakipendekeza huduma ya bima kufungamanishwa na baadhi ya huduma muhimu kama leseni ya udereva.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Akizungumza jijini Dar es Salaam, hii leo Septemba 27, 2022, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amebainisha kuwa utafiti walioufanya umebaini kuwa kati ya Watanzania 100 ni 15 pekee ndio wana bima ya afya, jambo linalosababisha asilimia kubwa ya wananchi kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Aidha Waziri Ummy amebainisha kuwa mwananchi atachagua bima ya afya ya gharama na huduma anazozitaka, huku akisisitiza kuwa elimu zaidi itaendelelea kutolewa kwa wananchi.