Bilionea Bezos aruka angani na roketi yake 

Jumanne , 20th Jul , 2021

Tajiri mkubwa duniani na Muanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Amazon Jeff Bezos amefanikiwa kwenda kwenye anga la juu zaidi na kurudi duniani ndani ya dakika 11 kwa kutumia roketi iliyotengenezwa na kampuni yake akivunja rekodi iliyowekwa na Bilionea Richard Branson mapema mwezi huu.

Roketi aina ya Blue Origin, ikiwa na Jeff Bezos na wafanyakazi ndani, ikiwa inapaa kutoka ardhini.

 

Bezos na pamoja na watu wengine watatu, walipaa na chombo maalum kisicho kuwa na rubani kwenda kwenye anga la juu zaidi duniani. 

Mnamo tarehe 11 Julai, 2021 Billionea Sir Richard Branson alifanikiwa kufikia ukingo wa anga za juu kutumia roketi ya Virgin Galactic na kuweka rekodi ambayo imevunjwa leo na tajiri mwenzake Jeff Bezos.

Tajiri Jeff Bezos na wenzake watatu wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kupaa angani