Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Bil. 79 kujenga vituo vya polisi kata nchi nzima

Alhamisi , 14th Mar , 2024

Serikali imedhamiria kutumia kiasi cha Tshs.Bilioni 79 kujenga Vituo vya Polisi Kata 698 katika maeneo mbalimbali nchini lengo ikiwa kutataua changamoto za kiusalama kwa jamii ambapo kila kituo kinatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 115.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni

Hayo yamebainika leo jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishwaji wa utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Vituo vya Polisi Kata ambapo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Jeshi la Polisi.

Ripoti hiyo ya utekelezaji imewasilishwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni huku ikihudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Adolph Ndunguru,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Maduhu Kazi, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Sospeter Mtwale na wataalamu kutoka pande zote zinazohusika na mradi huo.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema adhma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kumaliza tatizo la uhalifu kwa kulipeleka Jeshi la Polisi chini kwa wananchi na ndio maana amepandisha vyeo kwa ngazi ya nyota moja kwa askari katika maeneo mbalimbali nchini ili wakaongoze Vituo vya Polisi Kata na kushirikiana na wananchi katika dhana nzima ya kudhibiti uhalifu.

‘Rais Samia ametoa ajira na kupandisha vyeo askari akitaka jeshi lishuke chini kwa wananchi ili kuweza kupambana na uhalifu kuanzia ngazi ya kata kwa Tanzania Bara na ngazi ya Shehia kwa Zanzibar na ndio maana tunataka kuona mradi huu unaanza ili tuweze kufikia lengo husika,jamii ikon a wahalifu na inawajua ndio maana tunataka tusogee chini ili tuweze kusaidiana na jamii yae neo husika kudhibiti uhalifu.’ Alisema Waziri Masauni

Mradi huo utatekelezwa kwa fedha za Serikali kupitia Bajeti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI,wadau na mapato ya ndani ya Halmashauri husika kuanzia mwaka wa fedha 2024/25 mpaka 2026/2027 huku utaratibu wa force akaunti ambapo wataalamu wa Jeshi la Polisi, Halmashauri, Taasisi zingine za serikali, wananchi na wadau mbalimbali watatumika kutekeleza mradi.

HABARI ZAIDI

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ