Saimon Mtambo, katikati ni mke wake Fortunata Abraham, na kulia ni mtoto wakati wa uhai wao
Diwani wa Kata ya Kiwira, Michael Mwamwimbe, amesema huenda mauaji hayo yalitokea wiki tatu zilizopita na kwamba chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni mgogoro wa ndoa ambao umedumu kwa muda mrefu.
Aidha Mwamwimbe amefafanua kuwa watoto waliocharangwa mapanga na kisha kufariki dunia ni kijana wa kidato cha kwanza shule ya sekondari ya wavulana Busokelo na mtoto wa darasa la nne aliyekuwa anasoma shule ya msingi Ikuti iliyoko jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Rungwe, Dkt. Vicent Anney, amesema kuwa miili ya watu hao wanne imekutwa imeharibika na watazikwa kesho Septemba 15, 2022.

