Ijumaa , 14th Feb , 2025

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe. George Simbachawene amesema zaidi ya asilimia 40 ya Watumishi wa Umma hawafanyi kazi licha ya kulipwa mshahara kila mwezi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe. George Simbachawene amesema zaidi ya asilimia 40 ya Watumishi wa Umma hawafanyi kazi licha ya kulipwa mshahara kila mwezi.

Amesema hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na Tume ya Utumishi wa Umma nchini

Mhe. Simbachawene amesema hayo  leo  jijini Arusha wakati  akifunga Kikao kazi cha tano cha Serikali Mtandao ambapo amesema Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma wanawajibu wa kuhakikisha  kila mtumishi anatekeleza majukumu yake ipasavyo.

‘’Watumishi ni lazima wafanye kazi kwani wasipofanya kazi wanakuangusha wewe Mkuu wa Taasisi, lazima tuwe na jamii inayoandaliwa kufanya kazi’’ amesisitiza Mhe. Simbachawene

Amefafanua kuwa kwa mujibu wa tafiti hiyo, wavivu, wazembe, wagonjwa pamoja na waliosusiwa kutokana na vipaji na uwezo wao ni  asilimia 40 ya Watumishi wanaolipwa pasipo kufanya kazi

Amewataka Wakuu hao kuwatumia Watumishi wa Umma wenye vipaji na uwezo badala ya kuwafanyia fitina na hujuma hali inayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya nchi

Amesema hali hiyo imesababisha kutokuwepo kwa urithishanaji wa madaraka jambo ambalo limechangia kudhoofika kwa Taasisi pale kiongozi wa Taasisi anapostaafu au kuhama.