Muonekano wa gari aina ya Coaster baada ya kugongana na lori aina ya Mitsubishi Fuso
Ajali hiyo iliyohusisha magali mawili ambayo ni gari namba T.673 CUC aina Mitsubish Fuso iligongana na gari namba T.863 DXN Bus aina ya Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar es Salaam kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa mazishi.
Magari mawili aina ya Coaster na lori aina ya Mitsubishi Fuso baada ya kugongana
Mkuu wa Mkoa Wa Tanga Omary Mgumba amesema, chanzo cha ajali ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa gari Mistubish Fuso kulipita gali la mbele yake bila ya kuchukua tahadhari kulikosababisha kugongana uso kwa uso na Coaster.
Lori aina ya Mitsubishi Fuso baada ya kugongana na Coaster
Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospital ya Wilaya ya Korogwe na majeruhi 10 wamehamishiwa Hospital ya Mkoa wa Tanga Bombo na majeruhi wawili wamesalia katika Hospital ya wilaya ya Korogwe kwa matibabu.
Tukio la ajali baada ya kukaguliwa na polisi akiwemo RTO, magari yote yameshaondolewa barabarani kuruhusu barabara iendelee kupitika.
Tazama sehemu ya kipande cha video kwenye ajali hiyo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia ajali hiyo.
Nimesikitishwa na vifo vya watu 17 vilivyosababishwa na ajali iliyotokea jana saa 4:30 usiku eneo la Magila Gereza, Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga. Nawapa pole wafiwa na wote walioguswa na vifo hivi. Nawaombea ndugu zetu hawa wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka.
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) February 4, 2023