Ijumaa , 5th Aug , 2022

Ukosefu wa vifaa vya kisasa vya kuvulia samaki kwa wavuvi katika eneo la soko la samaki la Feri hasa katika kipindi hiki cha msimu wa baridi kumedaiwa kusababisha  wavuvi watatu kupotea baharini ndani ya kipindi cha mwezi wa  sita na mwanzoni mwa mwezi wa saba mwaka huu

Wakizungumza na EATV wavuvi hao wamesema kukosekana kwa vifaa vya uokoaii nako kumekuwa kukichangia wavuvi hao kuendelea kupotea baharini na kuziacha familia zao zikiteseka

Kwa upande wake mwenyekiti wa wavuvi katika soko la samaki Feri Ali Alawi amedai kwamba licha ya wavuvi hao kulipa fedha  nyingi za leseni ya uvuvi na kodi mbalinbali lakini wamekuwa hawathaminiwi wanapooatwa na matatizo baharini kutokana na kuendelea kutumia mitumbwi na ngarawa katika kuvua samaki baharini 

Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa kikosi Cha majini ACP Moshi Sokolo amesema kazi ya uokoaji baharini inaenda sambamba na kuwaokoa wavuvi pale taarifa inapowafikia mapema