Jumatatu , 12th Dec , 2022

Wananchi katika Kijiji cha Mbesa, wilayani Ruangwa mkoani Lindi, wamekiri kutofaidika na zao la Korosho kwa mwaka huu huku wakihofia suala la maandaalizi kwa watoto kwa ajili ya kuanza masomo kusua kwa sababu ya kupata fedha ndogo wakati huu wa mnada.

Korosho

Hayo wameyabainisha katika mnada wa 8 kwa muungano wa wakulima kutoka wilaya tatu za Ruangwa, Nachingwea na Liwale (RUNALI) na kusema kwamba bei ya korosho mwaka huu imewatupa mkono hivyo wanahofia hata shughuli zao binafsi kukwama kwa kukosa fedha.

Nao viongozi katika Kijiji na Halmashauri hiyo, wamesema kwa hakika bei imeshuka lakini kwa mnada huo wa mwisho hali si mbaya sana, huku wanakijiji wakihusiwa kutumia fedha vizuri ili waepukane na balaa la njaa ambalo linahisiwa kuwepo hapo mwakani.