Jumanne , 19th Jul , 2022

Mamlaka nchini Tanzania zimetangaza hatua zitakazochukua ili kuboresha uzalishaji wa miwa utakaosaidia kumaliza tatizo la uhaba wa sukari nchini humo.

Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo cha miwa ulioandaliwa na Bodi ya Miwa na kufanyika Morogoro, Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Hussein Bashe amesema, hatua hizo ni pamoja na ujenzi wa mifumo ya umwagiliaji kwa wakulima wadogo wa miwa katika maeneo ambayo kilimo hicho kinafanyika. 

Waziri huyo ametoa maelekezo kwa Bodi ya Miwa na Kamati ya Taifa ya Umwagiliaji kutambua maeneo katika mikoa inayolima miwa kwa ajili ya ujenzi wa mifumo ya umwagiliaji. Pia ametoa maelekezo kwa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Tanzania (TARI) kufanya utafiti wa mbegu bora za miwa.

Ametaja hatua nyingine kuwa ni kukusanya uzalishaji na matumizi ya mbegu bora za miwa ambazo zitazalisha mazao mengi.