Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

TPA Tanga yajipanga kushawishi wamiliki wa Meli

Ijumaa , 30th Dec , 2022

Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA mkoa Tanga imesema kuwa imeandaa mikakati ya kupunguza gharama kwa muda maalumu (Low Cost) ili kuwavutia wateja na kufanya mazungumzo ya kuwashawishi wamiliki wa meli kuanza kuleta meli kubwa bandari ya Tanga badala ya kutumia bandari jirani. 

Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha wakati waandishi wa habari za kiuchumi, biashara na uwekezaji walipotembelea bandari hiyo na kujionea maboresho yanayoendelea katika bandari hiyo.

Meneja Mrisha amesema serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), inatekeleza mradi huo mkubwa wa kimakakati wa maboresho makubwa katika bandari ya Tanga ili iweze kuchangia kikamilifu katika kukuza pato la Taifa kwa kuhudumia wateja wa ndani na nchi jirani ambazo zinategemea bandari za Tanzania kusafirisha bidhaa kutoka na kwenda nje ya nchi. 

"Mikakati yetu ya kimasoko baada ya kukamilika kwa ujenzi huu ni pamoja na kuitangaza bandari ya Tanga kwa kutumia vyombo vya ndani kama Radio na luninga na kuonyesha makala maalumu nje ya nchi kwa kutumia watumishi wa bandari waliopo nchi tunazohudumia, pamoja na Balozi zetu nchi mbalimbali kuitangaza bandari," amesema Mrisha. 

Kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika mradi wa maboresho ya bandari hiyo mradi huo utakapokamilika utakuwa na faida mbalimbali ikiwemo uwezo wa bandari ya Tanga wa kuhudumia shehena utaongezeka kutoka tani  750,000 mpaka tani 3,000,000.
 

HABARI ZAIDI

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi