
Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 7, 2021, kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, ambapo ameongeza kuwa serikali inao mpango wa kuhakikisha kuwa bidhaa ya mafuta inazalishwa kwa wingi hapa nchini kwa kuhakikisha inanunua mbegu mpya na zenye ubora wa kuzalisha mafuta mengi.
"Msisitizo wetu ni kwamba wafanyabiashara hasa hizi siku za mwisho za mfungo wa Ramadhan wasipandishe bei za mafuta, kesho ninakutana na waagizaji wote wakubwa wa mafuta Dar es Salaam ili tuzungumze kwanini mafuta yamepanda", amesema Profesa Kitila.
Aidha Profesa Kitila amongeza kuwa, "Serikali inatengeneza mazingira ili tupate mbegu mpya ambayo itakidhi mahitaji ya sasa kwa sababu kwa sasa mbegu tuliyonayo uzalishaji wake ni mdogo".