Alhamisi , 1st Dec , 2022

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Philip Basiimire amefurahishwa na namna ambavyo vipindi vinaendeshwa kupitia East Africa Tv na East Africa Radio huku akipongeza uwekezaji mkubwa uliofanyika katika urushaji wa matangazo.

Akizungumza hii leo Desemba 1, 2022 alipotembelea vyombo vya habari vya IPP jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa imekuwa siku nzuri ya kuimarisha ushirikiano baina ya Vodacom,  East Africa Tv na Eeast Africa Radio.

Aidha Mkurugenzi huyo kupitia kipindi cha Kipenga Xtra cha East Africa Radio kinachoruka kuanzia J tatu hadi Ijuma saa 6 mchana amesema yeye ni shabiki wa mpira na katika kipindi hiki cha michuano ya Kombe la Dunia yeye anashabikia timu ya Argentina.

Pia amepongeza namna ambavyo vipindi vinaendeshwa kisasa na kwenda sambamba na teknolojia kwani dunia kila siku inabadilika.