Alhamisi , 9th Feb , 2023

Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz kwa kushirikiana na benki ya Nbc wamekabidhi vyeti vya mafunzo ya bima kwa mawakala wa benki waliofanya mtihani na kufaulu mafunzo ya uuzaji wa bima yaliyoanza mwezi desemba mwaka 2022.

Mkurugenzi mkuu wa Jubilee Allianz Dipankar Acharya akikabidhi cheti kwa mmoja ya wahitimu wa mafunzo ya uuzaji Bima

Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz Awali ilichagua mawakala wa huduma za kifedha na kuwadhamini kupata mafunzo ya muda mfupi na sasa wako tayari kufanya biashara ya Bima ,ambapo ushirikiano huo unatarajia kutoa mafunzo kwa watu 6000 kufikia mwezi juni mwaka 2023.

“Mawakala ni viungo muhimu sana katika biashara ya bima hivyo tunaimani kwamba nyinyi mawakala mtakwenda kuwapa jamii elimu sahihi kuhusu bima” amesema Dipankar -Mkurugrnzi mkuu Jubilee Allianz.

Hata hivyo wamesema mafunzo hayo yatawawasaidia mawakala hao kufikisha taarifa sahihi kuhusu faida za bima na ni kwa jinsi gani mwananchi atazadi kunufaika kwa kuwa na bima mbalimbali.

Inchini Afrika kusini takwimu zinaonyesha asilimia 14 ya uchumi unatoka kwenye sekta ya bima hivyo wanaamini mafunzo hayo ya uuzaji bima yataongeza chachu katika kuongeza fursa za kibiashara.