EATV yakabidhi kapu la tatu wiki ya wateja

Alhamisi , 8th Oct , 2020

Kituo cha redio cha East Africa Radio kupitia kipindi chake cha Supa Breakfast kwa kushirikiana na Royal Oven Bakery kimekabidhi zawadi kwa mtoa huduma bora kutoka Silver ze smart dread’z, Silver Lonarick kufuatia kupata ushindi kwa kutoa huduma bora kwa wateja.

Muandaaji wa kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, Mackriner Siyovelwa akimkabidhi zawadi kutoka Royal Oven Bakery Silver Lonarick kutoka Silver ze smart dread’z.

Kampeni hiyo ya kuwazawadia watoa huduma bora katika Wiki ya Huduma kwa Wateja inaendeshwa kupitia wasikilizaji wa East Africa Radio ambao hupiga simu na kuelezea namna ambavyo dawati la kutoa huduma kwa mteja katika taasisi husika lilivyosaidia kutatua tatizo lao.

Akizungumza baada ya kupatiwa kapu hilo Silver Lonarick amesema kuwa mteja kwake ni mfalme na wamekuwa wakitoa huduma kwa hali ya upendo zaidi.

Kwakweli sikuamini kama ipo siku huduma ninayotoa kwa wateja wangu itapelekea kuzawadiwa tena na chombo cha habari kikubwa, nilikuwa nafikiria huwa wanapangwa watu kumbe kweli”, amesema Silver.

Kwa upande wake Muandaaji wa Kipindi cha Supa Breakfast Mackriner Siyovelwa baada ya kukabidhi zawadi hiyo ya kapu lililoshehena vitafunwa amewataka wasikilizaji kuendelea kupendekeza majina ya watoa huduma wao bora ikiwa kesho ndio kilele.