Jumatatu , 14th Nov , 2022

Kampuni ya Coca Cola kwanza kupitia kampeni yake ya Biriani friday na Coka imedaiwa kuwawezesha vitendea kazi migahawa ya wajasiriamali zaidi ya hyamsini 50 ambao hujihusisha na kuandaa biriani kila ijumaa kwa mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro,Tanga Mtwara,Zanzibar na Mbeya.

Akieleza madhumuni ya uwezeshaji huo meneja biashara na masoko wa kampuni hiyo Wahida Mbaraka amesema kwa sasa uwezeshaji huo unaelekea makao makuu ya nchi Dodoma ili kuifungua fursa hiyo.

“Wakazi wa Dodoma tunakuja na safari hii wapishi wa biriani kumekucha tutawakutanisha na wateja wenu na watapata nafasi ya kupata Coka naq sisi tutawawezesha vifaa ili wakidhi mahitaji yao kiuchumi huku wakipata burudani safiii” amesema Wahida Mbaraka- Meneja Biashara na Masoko Coca cola Kwanza.

Biriani festival na coka itawakutanisha wapishi wa biriani na wateja wao leongo ikiwa ni kuchagiza vyakula vya asili vya mkoa wa Dodoma kutokana na mkoa huo kuwa na muingiliano mkubwa wa watu wenye asili tofauti.

Hivi karibuni kampuni hiyo iliwawezesha wajasirimali wa chips zaidi ya 900 kwa mkoa wa Dar es Salaam majiko ya gesi mitungi, meza,pamoja na kuwapatia mafunzo ya kutunza kumbukumbu sahihi za fedha lengo ikiwa ni kuona vijana wanakuza mitaji na kuinuka kiuchumi.