PRESENTERS

Menina Atik
+

Meninah Atik ni mwanamuziki chipukizi, mtunzi wa nyimbo na dancer.

Amezaliwa Tarehe 18/03 na kupata elimu ya sekondari Kenton na kwa sasa ni mwanachuo, Dar es Salaam University School of Journalism (DSJ), akisomea Shahada yake ya kwanza kwa masomo ya Mass Communication.

Menina anapenda movies, kusoma novels, kuogelea na kusafiri kwa njia ya gari (road trips)

Anapendelea sana kukaa nyumbani kuliko kutoka out.

Colorbox trigger:
TBway 360
+

Jina halisi ni Tony Albert.

Amezaliwa Tarehe 10/06 Mwanza na kukulia ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Amesoma shule za Esaacs Primary School na Kampala International High School.Tbway ana urefu wa futi 6.5

Anapenda sana kupiga picha, kuogelea, movie na kuendesha magari kwa kasi.

Alipachikwa jina la TBWAY 360 akiwa na umri wa miaka 14 baada ya kuzungusha gari mzunguko wa duara yaani nyuzi 360

Colorbox trigger:

Sponsored BY

JUDGES

LOTUS KYAMBA
+

Mtangazaji wa EATV kipindi cha Nirvana.

Amezaliwa Tarehe 19/08 Dar es Salaam, na kulelewa jiji la Stockholm, Sweden.

Ni mwanadada machachari sana mwenye style ya maisha ya kipekee kabisa.

Lotus ni dancer pia na akiwa kama judge Lotus, hatabiriki kabisa.

SUPER NYAMWELA
+

Jina Kamili anaitwa Hassani Mussa Mohamed.

Amezaliwa Pundula mkoani Ruvuma, Tarehe 08/06.

Ni Dancer mkongwe anayecheza ndani ya bendi ya Extra Bongo, Mwanamuziki na pia ni Raisi wa Chama cha Dancers Tanzania.

**Katika majaji wote, judge huyu ndio mkali na asiyetoa maksi kubwa kirahisi.

QUEEN DARLEEN
+

Jina lake halisi anaitwa Mwanahawa Abdu Juma.

Amezaliwa na kulelewa Ilala, Dar es Salaam.

Ni msanii wa muziki miaka mingi na mwenye swagg za kigumu kidogo na kidada kidogo.

Hapendi Kokoro.

Anapenda kula, kuogelea, kuimba na kucheza.

ARTICLES

Kundi la Wakali Sisi Likikabidhiwa Hundi pamoja na Kombe na zawadi zao na Meneja Uhusiano wa Umma kutoka Vodacom, Bwana Matina Nkurlu

4 Oct . 2014

Washindi wa leo wakiwa pamoja baada ya kutangazwa kushinda kuingia hatua ya fainali.

13 Sep . 2014

Kundi la Quality Boys likiwa linaonyesha uwezo mbele ya majaji leo

23 Aug . 2014

shindano la Dance100% 2014 nchini Tanzania

4 Aug . 2014

Moja ya Makundi yaliyojitokeza leo TCC Chang'ombe yakionyesha uwezo mbele ya majaji

3 Aug . 2014

Pages

Dance 100% ni event ya nguvu kinoma ambayo huandaliwa na kituo cha television cha EATV na hufanyika kila mwaka kwa muda maalum uliopangwa.

Event hii iko kimtaani zaidi, maana hutembelea mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kuweka vituo vvyake kwaajili ya kufanya usajili wa makundi ya wachezaji (dancers) ambao wanapenda kucheza, kisha baada ya hapo hufanya mchujo katika vituo hivyo na kuchukua makundi matano ya washindi toka katika kila kituo na kuwapambanisha pamoja.

Lengo kuu la event hii ni kuwakutanisha vijana mbalimbali wenye uwezo wa kucheza ,na kisha kuwafanya wajulikane na watu tofauti kupitia kipindi hiki.

Washindi wanaopatikana katika event hii huzawadiwa fedha taslimu na zawadi nyinginezo kama zipo, kwa kuwapa zawadi washindi hawa huwafanya waweze kununua vifaa mbalimbali wanavyoviitaji katika sanaa yao na pia kuweza kufanya mambo yao mengine tofauti.

Dancers katika event hii hucheza nyimbo mbalimbali zikiwemo reggae, R&B, Hip Hop na nyinginezo, na pia ili mtu aweze kushiriki anapaswa awe na kikundi cha wenzake, mwenye afya njema, umri wa kuanzia miaka 18 (kama ana chini ya miaka hiyo anapaswa aje ana kibali toka kwa wazazi)