Jumamosi , 4th Oct , 2014

Fainali ya mashindano makubwa kabisa ya kudansi Afrika Mashariki, Dance 100 2014, yamefanyika leo kwa mafanikio makubwa na kundi la Wakali Sisi kufanikiwa kuibuka kidedea katika nafasi ya kwanza kama wakali wa kudansi kwa mwaka huu.

Kundi la Wakali Sisi Likikabidhiwa Hundi pamoja na Kombe na zawadi zao na Meneja Uhusiano wa Umma kutoka Vodacom, Bwana Matina Nkurlu

Kundi hili limekabidhiwa hundi ya shilingi Milioni 5 kama zawadi kuu ya mshindi, Smartphone aina ya Vodaphone zikiwa na muda wa maongezi shilingi Laki 1 kwa kila mwanakundi, pamoja na Kombe, huku mshindi wa pili The WT akiondoka na hundi ya shilingi Milioni 1 na laki 5, na mshindi wa tatu kundi la Wazawa Crew akiondoka na zawadi ya hundi ya shilingi laki 5.

Hii ni baada ya mpambano mkali wa round mbili kwa kila kundi, hatua ya kwanza ikihusisha kucheza Mega Mix za makundi ana ya piali ikihusisha kucheza nyimbo maalum ambazo ziliandaliwa na waratibu na makundi haya kujichagulia yenyewe.

MAshindano haya pia yamehusisha burudani ya aina yake ambapo katika hatua ya Ufunguzi, washiriki wote walipata nafasi ya kudansi na Msanii Mahiri na mwalimu wa Dansi Msami, kbla ya msanii huyu na timu ya madansa wake kulishambulia jukwaa kwa ku-perform nyimbo zake zinazofanya vizuri ikiwepo Soundtrack.

Vilevile baada ya mzunguko wa pili mkali wa kusuka mabiti na msanii Mesen Selekta naye alilishambulia jukwaa na kufanya live hits zake kali kabisa ikiwepo Kanyaboya.

Majaji wa mashindano haya kama kawaida walikuwa ni Super Nyamwela, Lotus kutoka EATV na Queen Darleen, na washereheshaji wakiwa ni T Bway pamoja na msanii wa muziki mkali kabisa Meninah.

Mashindano haya kwa ujumla wake yamewapambanisha makundi 5, wakiwepo Wakali Sisi, The Winners, Wazawa Crew, The WT pamoja na Best Boys yakidhaminiwa kwa nguvu na Vodacom Tanzania pamoja na Grand Malt.

Kundi la The WT lililokamata nafasi ya Pili wakikabidhiwa zawadi zao
Kundi la Wazawa Crew likikabidhiwa hundi yao na Bwana Kulwijira Maregesi kutoka BASATA