Jumatatu , 4th Aug , 2014

Usaili wa mwisho wa shindano la Dance100% 2014, umemalizika kwa kishindo jana katika uwanja wa TCC Chang'ombe Jijini Dar es Salaam.

shindano la Dance100% 2014 nchini Tanzania

Kutokana na mpambano mkali, jumla ya makundi 6 yaliyojitokeza katika usaili huo wa mwisho yameweza kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali.

Makundi yaliyoweza kushinda kupita katika usaili huu ni The WT, Best Boys Crew, Bad Crew, Best Love na WAZAWA ambao walifungana alama na G.O.P., na hivyo kusababisha makundi haya mawili kupata nafasi ya kusonga mbele pamoja na kufanya jumla ya makundi yaliyopita jana kuwa 6.

Kwa sasa makundi yote yaliyopita kutoka Don Bosco Upanga, Don Bosco Oysterbay na TCC Chang’ombe, ni 16 ambayo yanajifua kujiadaa kwa mpambano mkali zaidi wa hatua ya robo fainali itakayoanza hivi karibuni.

Kwa kutazama kilichojiri jana, usikose show hii kali inayokwenda kwa swaga ya Dance 100% 2014 kupitia EATV, siku ya Jumatano saa 1 kamili jioni.