Jumamosi , 23rd Aug , 2014

Hatua ya robo fainali ya shindano kubwa kabisa la Kudance la Dance 100% 2014, yamefanyika leo katika uwanja wa Don Bosco Oysterbay ambapo makundi 16 yamepambana mbele ya majaji na hatimaye kupata makundi 10 ambayo yanasonga mbele nusu fainali.

Kundi la Quality Boys likiwa linaonyesha uwezo mbele ya majaji leo

Makundi ambayo yamefanikiwa kusonga mbele katika mashindano haya ni pamoja na Quality Boys, Dar Crew, Best Boys, The WT, The Winners Crew, Wakali Sisi, Tatanisha Dancers, GOP, Wazawa Crew na Mazabe Powder.

Kivutio kikubwa katika mashindano haya leo ni namna ambavyo makundi yameweza kuonyeshana uwezo sambamba na burudani mbalimbani, ikiwepo onyesho za sarakasi na ujuzi wa kucheza na baiskieli kutoka kwa vijana wa Grand Malt, zawadi mbalimbali zikitolewa kwa mashabiki zikiwepo kofia na Tshirt kutoka kwa wadhamini Vodacom na EATV pia.

Unaweza kufuatilia kilichojiri katika mashindano haya kupitia www.twitter.com/eastafricatv ama tembelea https://eatv.tv/shows/dance-100 na pia na kwa kutazama kilichojiri leo, usikose show kali ya Dance 100% kupitia EATV, Jumatano saa 1 kamili jioni.

Kwenda sambamba na mashindano haya katika mitandao ya kijamii, tumia #2014Dance100

Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mpambano wa kudansi leo
Kundi la B2K likiwa linaonyesha uwezo wake mbele ya majaji