Jumamosi , 13th Sep , 2014

Baada ya mchuano Mkali, Makundi 5 ya kudance, Wakali Sisi, Wazawa Crew, Best Boyz, The WT, na The Winners yamefanikiwa kuingia katika hatua ya fainali ya mashindano makubwa kabisa ya kudansi Afrika Mashariki, Dance 100% 2014.

Washindi wa leo wakiwa pamoja baada ya kutangazwa kushinda kuingia hatua ya fainali.

Tukio la kipekee pia kutoka katima mashindano haya ni rekodi iliyowekwa na kundi la Wazawa kwa kupata maksi 100 kutoka kwa jaji Super Nyamwela baada ya ubunifu wao kufurahisha wengi na kumgusa jaji huyu kipekee.

Makundi yaliyoshiriki hatua hii ni Quality Boys, Wakali Sisi, The Winners, Tatanisha Dancers, Mazabe Powder, The WT, Best Boys, Wazawa Crew, Dar Crew na G.O.P ambao waliingia uwanjani kwa mizunguko miwili, moja wakiwa wanacheza Megamix zao nay a pili wakiwa wanacheza nyimbo walizoandaliwa na kuzichagua wenyewe.

Mashindano haya yamefanyika leo na kuleta burudani ya aina yake kwa umati mkubwa wa mashabiki waliohudhuria katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kwa kufuatilia kilichotokea leo usikose kutazama show kali ya Dance 100% kupitia EATV siku ya Jumatano saa 1 kamili jioni.