Jumapili , 3rd Aug , 2014

Shindano Dance 100% 2014, limemaliza usaili wake wa Tatu na wa mwisho katika viwanja vya TCC Chang’ombeTemeke Jijini Dar kwa mafanikio makubwa likishihudia makundi Zaidi ya 10 yakijitokeza kuwania nafasi ya robo fainali ya mashindano hayo.

Moja ya Makundi yaliyojitokeza leo TCC Chang'ombe yakionyesha uwezo mbele ya majaji

Makundi yaliyojitokeza kushiriki ni pamoja na The Sun Flag, Bad Dancers, Virus, Dar Crew, Best Boys Crew, Street Dancers, Manuary, GOP, B-13, MWANZO Mpya na Butterfly.

Makundi yaliyoweza kushinda kupita katika usahili huu ni The WT, Best Boys Crew, Bad Crew, Best Love na WAZAWA ambao walifungana alama na TOP, na hivyo kusababisha makundi haya mawili kupata nafasi ya kusonga mbele pamoja na kufanya jumla ya makundi yaliyopita leo kuwa 6.

Onesho hilo limepewa hype ya kutosha na Kennedy The Remedy, Dickson Msami, pamoja na kuendeshwa na watangazaji T Bway 360 pamoja na Meninah likiwa na udhamini mzito wa Vodacom Tanzania na Grand Malt.
Kwa sasa makundi yote yaliyopita kutoka Don Bosco Upanga, Don Bosco Oysterbay na TCC Chang’ombe ambayo idadi yake jumla ni 16, yanajiamdaa kwa mpambano mkali Zaidi hatua ya Robo Fainali.

Kwa kutazama kilichojiri leo, usikose show kali ya Dance 100% kupitia EATV, Jumatano saa 1 kamili jioni.