Makamu wa rais ahimiza mapambano dhidi ya rushwa
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewakumbusha Watanzania kuwa wazalendo na nchi yao ikiwa ni pamoja na kukataa matendo ya kutoa ama kupokea rushwa ili kudumisha haki na usawa katika Taifa.