Marketers Night
Marketers night ni usiku wa mkusanyiko wa wafanyabiashara mbalimbali jijini Dar es salaam.
Usiku huu unashirikisha Afisa masoko kutoka pande mbalimbali za jiji kwa kuwaleta pamoja kwa nia ya kubadilishana mawazo na kukuza wigo wakufanya biashara.
Katika mkusanyiko huo wafanyabiashara hupata semina mbalimbali za kukuza biashara na kupanua wigo wa mawasiliano na nyanja za biashara katika makampuni tofauti.
Katika hafla hiyo inayoambatanishwa na chakula na vinywaji huwapa wafanyabiashara mandhari nzuri ya kujuana na kubadilishana mawazo na changamoto mbalimbali.