Mutungi aonya kuhusu vikundi vya ulinzi na usalama
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa nchini kuvivunja vikundi vyao vya ulinzi na usalama kufuatia vyama hivyo kukiuka sheria za nchi kwa kuanzisha mafunzo ya kijeshi kwa vikundi hivyo.

