Stars kujipima kabla ya kuvaana na Misri
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inaweza kucheza mchezo mmoja wa kirafiki nchini Ethiopia kabla ya kwenda kumenyana na Misri wiki ijayo, mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika.