Monday , 22nd Jun , 2015

Ili kuibuka na ushindi mkubwa na kuweza kumchagua kiongozi Bora kutoka ndani ya chama cha mapinduzi watanzania wametakiwa kuzitunza shahada za kupigia kura ifikapo octoba 25 mwaka huu.

Waziri mkuu wa Zamani Mh. Edward Lowassa.

Hayo yamesemwa na Waziri mkuu wa Zamani Mh. Edward Lowasa wakati akiwa mkoani Njombe kutafuta wadhamini ambapo amepata zaidi ya watu elfu kumi kutoka katika wilaya zote sita za mkoa huo.

Mh. Lowassa amewaambiwa wananchi wa Mkoa wa Njombe pindi watakapopoteza shahada ya kupigia kura watakakuwa wamepoteza haki yao ya msingi ya kuweza kumchagua kiongozi bora kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Lowasa amesema kuwa kitendo cha serikali kuchelewesha fedha za wakulima wa mahindi mkoani njombe kimetokana na uzembe wa serikali na kwamba kama ataingia madarakani hatakuwa tayari kuona kinaendelea.

Aidha Ameendelea kusimamia falsafa yake ya kuuchukia umasikini kwa kuwataka watanzania wamchague ili aungane nao kuutokomeza.