DAWASCO washauriwa kufunga mita za kulipa kwanza
Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini Tanzania Profesa Makame Mbarawa ameliagiza Shirika la Maji Safi na Maji Taka Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) kuona namna ya kuweka mita za maji ambazo mteja hatoweza kutumia maji iwapo hajalipia kwanza (Prepaid).