Dhima ya mapinduzi ni kuboresha huduma za kijamii
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa hatua za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba za kuimarisha huduma za afya za vijijini ni miongoni mwa utekelezaji wa shabaha ya mapinduzi.