Friday , 15th Jan , 2016

Wanamgambo wa kundi la Islamic State wamedai kuhusika na shambulizi la Alhamis katika mji mkuu wa Indonesia wa Jakarta shambulizi ambalo lilisababisha vifo vya watu saba wakiwemo washambuliaji watano.

Msemaji wa polisi wa Indonesia, Anton Charliyan alisema kundi lenye uhusiano na IS huwenda lilihusika na shambulizi hilo na washambuliaji walionekana kujaribu kufuata mashambulizi ya ugaidi yaliyofanyika mwezi Novemba mjini Paris nchini Ufaransa.

Hata hivyo Shirika la habari la Aamag lenye uhusiano na wanamgambo wa Islamic State-IS lilisema shambulizi katika mtaa wa matajiri wa Jakarta liliyalenga mataifa ya kigeni na vikosi vya usalama vinavyofanya kazi kuwalinda.

Chanzo Voa