TRA yatakiwa kudhibiti ubadilishaji fedha mpakani
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameitaka Mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Mbeya kuhakikisha inaandaa mpango maalum kwa ajili kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na biashara ya ubadilishaji wa fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma.

