Sina taarifa ya uwepo wa 'mazombi' Z'bar-Seif Idd
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema hana taarifa zilizomfikia kama kiongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi, kuhusiana na kuwapo kwa kikundi cha vijana wanaopiga watu katika baadhi ya maeneo, maarufu mazombi.
