Zitto Kabwe aunga mkono 'utumbuaji majipu'
Mbunge wa Kigoma mjini kupitia Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe amesema kuwa chama chake kinamuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika jitihada zake za kukabiliana na ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

