Zitto ameyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa kuhusu kikao cha kamati ya chama chake kwa wanahabari ambapo amemtaka Rais kugeukia pia posho za watumishi wa umma.
''Rais anatakiwa kugeukia suala la posho, afute posho za vikao kwa mfumo wa watumishi wa umma, ikiwamo bunge na kuachana na matumizi ya magari ya anasa ili kusaidia kuleta maendeleo''.
Aidha Zitto amesema kuwa kamati kuu ya chama chake ilipokea na kujadili utendaji wa serikali ya awamu ya tano na kuunga mkono juhudi za kupambana na rushwa na ufisadi nchini kupitia dhana ya ‘kutumbua majipu'




