Saturday , 23rd Aug , 2014

Wasanii wa muziki wanaofanya kazi chini ya studio ya Tongwe Records, wamechukua hatua ya kumfariji mtayarishaji muziki J Murder kwa kuondokewa na baba yake, Jaji Lewis Makame kwa kutunga wimbo wa maombolezo.

Jeneza la Marehemu Jaji Lewis Makame

Kwa niaba ya wasanii wenzake, Walter Chilambo ambaye naye pia ameshiriki katika kazi hii amesema kuwa, wamemfahamu Jaji Lewis Makame kama mtu muungwana na smart ambaye amekuwa mzazi muelewa kwa kile wanachokifanya na mwanae J Murder kama wasanii.

Maziko ya Jaji huyu ambaye amekuwa na mchango mkubwa Serikalini yamefanyika siku ya leo huko Tanga.

Mungu ailaze roho ya marehemu Mahala Pema Peponi aamin.

Mtayarishaji muziki J Murda (Kushoto) akipata faraja kutoka kwa Rais Kikwete kwa pigo la Msiba
Marehemu jaji Lewis Makame